Huduma ya choo imerejea katika choo cha Stand kuu ya mabasi Shinyanga kufuatia huduma hiyo kusimama kwa masaa matatu na kusababisha usumbufu kwa wasafiri na wafanyabiashara wanaotumia choo hicho hali iliyopelekea serikali kuchukua hatua za dharura kwa kutafuta maji katika vyanzo vingine.
Akizungumza na Jambo Fm kuhusiana na tukio hilo mstahiki meya wa halmashuri ya manispaa ya Shinynga Elias Masumbuko amesema kuna upungufu ya maji katika maeneo mengi ya manispaa ya Shinyanga likiwemo eneo hilo la stand kutokana na chanzo cha maji kilichopo Iherere jijini Mwanza kujaa tope hivyo kuwalazimu kuchukua hatua za dharura kwa kutafuta maji katika maeneo mengine.
Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamelalamikia hatua ya hapo awali ya kukosekana kwa huduma ya choo katika eneo hilo huku wakiiomba serikali kusimamia upatikanaji wa maji hususani katika maeneo hayo kwani hali hiyo inaweza kusababisha magomjwa ya mlipuko , kutokana na wao kujisaidia eneo la makaburi jirani na stand hiyo pindi vyoo hivyo vinapofungwa kutokana na ukosefu wa maji.