HOTUBA YA RAIS SAMIA IMEGUSA MATARAJIO YETU – BABA, MAMA LISHE SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Mama na Baba Lishe wa Manispaa ya Singida, wamepongeza hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakisema imegusa changamoto na matarajio yao kwa kina.

Wamesema kupitia hotuba ya Rais Dkt. Samia kuna masuala mbalimbali ambayo yatawaongezea heshima, kuimarisha motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kuboresha taswira ya biashara zao katika jamii, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali.

Aidha kwa upande wake Kaimu KatibuTawala wa Mkoa wa Singida Donatila Vedasto akizungumza na washiriki wa Mama na BabaLishe Mkoani humo , Kaimu Katibu Tawala amewataka kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo ya Rais kwa ajili ya kuboresha utendaji wao.

Amesisitiza, kuwa ni wajibu wa Mama na Baba Lishe kuhakikisha wanatumia fursa kupitia shuguli zao kwa kujipanga upya na kuboresha huduma zao kwa wateja wanaowahudumia ili kuendana na mabadiliko chanya na kukua kichumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *