Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Hospitali wa Apollo kujengwa nchini

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza wizara ya afya kufufua mchakato wa mazungumzo wa ujenzi wa Hospitali ya Apollo nchini na kuelekeza Mfuko wa Hifadhi za Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuona njia watakazoweza kushirikiana kutekeleza ujenzi wa Hospitali hiyo kwa kushirikiana na wizara ya afya.

Rais Samia amesema hayo kufuatia mazungumzo baina yake na Mwenyekiti mwanzilishi wa Hospitali za Apollo nchini India, Dkt. Prathap Reddy kwa njia ya mtandao ambapo mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Mkurugenzi wa Hospitali za Apollo, Sangita Reddy. Kwa upande wake Dkt. Reddy ameahidi kuanza utekelezaji wa mradi wa hospitali hiyo jijini Dar es Salaam kwa awamu na utelezaji wake utaanza mara moja endapo Serikali itakamilisha hatua zote zinazotakiwa katika mchakato wa ujenzi huo.

Mtandao wa Hospitali wa Apollo una Hospitali zaidi ya 73 duniani, tangu kuanzishwa kwake imeshatoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa milioni 150 kutoka katika mataifa zaidi ya 140 duniani.

Ujenzi wa Hospitali hiyo hapa nchini ni juhudi za dhati za Rais Samia katika kuboresha huduma za kibingwa na kibobezi kupatikana karibu zaidi kwa Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *