Hofu ya mastaa kubeba kunguni ya tawala

Wiki ya Mitindo ya Paris imeisha, lakini kuna hofu kubwa imetanda kwa mastaa waliofika kwenye maonyesho hayo kuondoka na wadudu aina ya Kunguni wanaotajwa kuwa tishio ndani ya mji wa Paris- Ufaransa.

Dk. Jim Fredericks, mtaalamu wa wadudu aliyeidhinishwa na bodi na Makamu Mkuu wa Rais wa masuala ya umma katika Chama cha Kitaifa cha Kudhibiti Wadudu, amebainisha kuwa kunguni waliokuwa katika vitanda vya hoteli walivyolala mastaa wana uwezekano wa kupata nafasi ya kuingia Marekani wakitokea Paris.

Hivyo amewataka mastaa hao kufanya ukaguzi mkali wa mizigo yao lakini pia kwenye majumba yao hasa sehemu wanazo lala na pia kujikagua miili yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *