
Kwa mujibu wa tovuti ya BBC Swahili iliyochapishwa Agosti 21 2021 ilitaja vyakula ambavyo kwa binadamu ikitokea vimechanganywa vina uwezo wa kugeuka na kuwa sumu kwa Mwanadamu pale atakapovitumia.
Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna aliiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote, Vyakula hivyo ni Pamoja na

Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shida baadaye, Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja zilizochanganywa na hii huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.
Kingine ni Maziwa na Limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yatakatika, ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana, karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile Karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito, kwa mafuta ya mzeituni yana msaada mkubwa hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaweza kuleta shida lkn inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio vyote kwa pamoja.
Kingine ni kuamua kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama soda za machungwa au jamii ya Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.
Mtaalam aliongeza kwa kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa ni hatari. Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu. Inaweza kuwa sumu kwa wengine, Upande mwingine inaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo kwa Pamoja, Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.
Mtaalamu anasema kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio hujenga mwili.
“Mayai mabichi sio ya kuyaamini,” Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba Haruna, Hiyo pishi linalohusisha mayai mabichi na nyama mbichi linaweza kuwa hatari kwa afya.
Wataalamu wanashauri watu kula kile chakula wanachokijua chenye faida na haitawasababishia matatizo yoyotelakini Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara.