Hili Lilichangia Watoto Wetu Kushindwa Kuendelea na Shule

Costantine James,Geita

Wananchi katika Kata ya Ipalamasa wilayani Chato Mkoani Geita wameishukuru serikali kwa kuwaondolea changamoto ya watoto wao kusafiri maeneo mbalimbali nchini kusaka elimu baada fedha kutolewa ili kutekeleza mradi wa uboreshaji wa shule ya sekondari Ipalamasa hatua itakayowezesha shule hiyo kuwa na madarasa ya kidato cha tano na sita.

Wamebainisha hayo wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Chato Said Nkumba aliyoifanya kwa lengo la kukagua maendeleo mradi huo wakieleza kwamba kukamilika kwake kutawapunguzia gharama walizokuwa wakizitumia hali ambayo wakati mwingine ilikuwa ikisababisha watoto kushindwa kuendelea na masomo na sasa changamoto hiyo itatuliwa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Mandia Kihiyo amesema ili kumaliza changamoto ya wakazi hao serikali imetoa milioni 853 kwa lengo la kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 wanaotarajiwa kuanza masomo mwaka huu katika shule hiyo.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo mkuu wa wilaya ya chato Said Nkumba amewataka wafundi wote wanaotekeleza ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano na sita katika wilaya hiyo kuhakikisha ifikapo Juni 25 mafundi wote wawe wamekabidhi miundombinu hiyi ili kutoa nafasai kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo katika shule hizo kuanzia julai mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *