Hiace yapinduka na kuua wanne Bukoba

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 21 wamejeruhiwa kwenye ajali ya barabarani baada ya basi dogo la abiria aina ya Hiace kupinduka katika eneo la Kyetema, lililopo katikati ya Kata za Bujugo na Kemondo, wilayani Bukoba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Blasius Chatanda amesema ajali hiyo imetokea leo Disemba 5, 2023 majira ya saa 5.00 asubuhi na kuwa Hiace hiyo ikiwa na abiria, ilikuwa ikitokea Kata ya Izimbya ikielekea Bukoba mjini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *