Bingwa mara mbili wa dunia wa riadha mkenya Hellen Obiri (34) jana jioni ameibuka mshindi wa kwanza wa mashindano ya 128 ya riadha ya Boston upande wa wanawake akikimbia maili 26.2 kwa muda wa saa 2:22:37 kutoka Hopkinton Center hadi Copley Square.

Huu ni ushindi wake wa pili mfululizo wa mashindano ya Boston, ambapo anakuwa mwanamke wa kwanza tangu mwaka 2005 kushinda mara mbili mfululizo mashindano hayo, baada ya mkenya mwenzake Catherine Ndereba kufanya hivyo hiyo mwaka 2005.
Kwa ushindi huo Hellen amejinyakulia zawadi ya ushindi ya kitita cha Dola za marekani 150,000 ambazo ni sawa na Tsh. 387,000,000/=.
Kwa upande wa Wanaume Sisay Lemma (33) raia wa Ethiopia ambaye ni mwanaume wanne aliyekimbia haraka katika historia baada ya kumaliza kwa muda wa saa 2:01:48 kwenye Valencia Marathon mwaka jana, ameibuka mshindi kwa kukimbia muda wa saa 2:06:17, nae amejinyakulia zawadi ya ushindi ya kitita cha Dola za marekani 150,000 sawa na Tsh. 387,000,000.

