Helikopta Yakatisha Maisha ya Rais na Waziri wa Mambo ya Nje Iran

Serikali ya Iran imethibitisha kifo cha Rais wake, Ebrahim Raisin, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na maofisa wengine kadhaa waliofariki katika ajali ya helikopta Mei 19, 2024 usiku wa kuamkia leo.

Ajali hiyo imetokea kaskazini-magharibi mwa Iran, kwenye mteremko wa mlima katika eneo la Varzaghan, karibu na mpaka wa Azerbaijan Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, hali mbaya ya hewa imetajwa kuwa sababu ya kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha shughuli za uokozi kukabiliwa na upinzani kwa takribani zaidi ya masaa 12.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *