Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa awamu ya pili, ametunukiwa tuzo ya heshima kutokana na mchango wake kukiendeleza lugha ya Kiswahili nchini na kimataifa.
Tuzo hiyo imetolewa Machi 18,2024 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika Mbeya.
kwa niaba ya familia, tuzo hiyo imepokelewa na Abdullah Mwinyi ambaye ni mtoto wa hayati Mwinyi, mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.