Haya ndio maisha ya Tory Lanez, Jela

Hizi ndio ripoti za mwanetu Tory Lanez, anavyoishi  maisha yake kwa sasa ndani ya Jela ya Los Angeles, ambapo amewekwa mbali na watu wa kawaida na anapata saa chache tu kwa siku kuwa nje.

Tory anaruhusiwa kutoka kwenye seli yake kwa saa 2 sawa na dakika hizo 120, pia anaruhusiwa kupata hewa safi wakati wa kutafakari kwa saa 3 pekee kila wiki

Kwa mujibu wa utekelezaji wa sheria, Tory anaingia kwenye kile kinachoitwa kitengo cha ubaguzi wa kiutawala, ambacho ni cha wafungwa ambao hawawezi kuwekwa salama pamoja na watu wengine gerezani. Rapa huyo anatumika kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi Megan Thee Stallion mnamo 2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *