HAWA NDIO WACHEZAJI WA YANGA WATAKAOKOSEKANA KWENYE MCHEZO WA MARUDIANO NA TP MAZEMBE ….

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ndani ya Klabu ya Yanga, imesema kuwa Yanga itawakosa Mastaa wake kadhaa, akiwemo Maxi Nzengeli, Clatous Chama, Yao Kouassi na Aziz Andabwile kwenye mchezo wao wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Taarifa ya Yanga inasema kuwa Chama bado anaendelea na matibabu ya jeraha la mkono huku Yao akiendelea na matibabu ya jeraha la goti.

Maxi na Andambwile tayari wameshaanza mazoezi lakini bado hawajawa tayari kwa mchezo wa kesho utakaochezwa kuanzia saa kumi jioni.

katika msimamo wa kundi A Yanga iko nafasi ya mwisho ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu, ikipoteza miwili na kutoa sare moja. Kama ambavyo msimamo wa kundi hilo ulivyo.

Msimamo wa kundi A
1.Al Hilal- 9
2. MC Alger- 4
3. TP Mazembe – 2
4. Yanga – 1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *