HAWA NDIO MAKAMISHNA WAWILI WA POLISI WALIOTEULIWA NA RAIS SAMIA DISEMBA 9 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Makamishna walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Kombo Khamis Kombo amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, anachukua nafasi ya CP. Hamad Khamis Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Balozi; na

(ii) Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Tatu Rashid Jumbe amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi, anachukua nafasi ya CP. Suzan Kaganda ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *