Klabu ya Liverpool imefuta uvumi ulikouwa ukiendelea juu ya mshambuliaji kinara wa timu hiyo Mohamed Salah.
Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari za michezo zilieleza kuwa Salah anawindwa vikali na klabu kutoka nchini Saudi Arabia, ambapo klabu ya Al- Ittihad ilitajwa kuandaa dau nono la usajili wa nyota huyo na kumfanya kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi katika ligi hiyo.
Liverpool ambao ndio waaajiri wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, wamefuta uwezekano wa usajili huo kukamilika wakisema hawana mpango wa kuumuza Salah na hawapo tayari kusikiliza ofa yoyote juu ya nahodha huyo wa Misri.