Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa hakitasusia maridhiano na vyama vya upinzani nchini kwenye jambo lolote la kujenga na lenye maslahi kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na wanachama alipowasili kwa mara ya kwanza Makao Makuu Dodoma tangu kuteuliwa.