HATUJAWAHI KULA HATA SENTI YA WHOZU- FRED VUNJA BEI.

Muda mfupi toka msanii wa muziki wa Bongo Fleva Whozu kutoka hadharani na kuufahamisha umma kuwa hafanyi kazi tena na lebo yake iliyomtoa ya TOO MUCH MONEY, Leo miongoni mwa Wakurugenzi wa lebo hio Fred Vunja Bei ametoka na kutoa taarifa.

Kupitia ukurasa wa instagram Fred Vunja Bei ameandika ‘Frank na Mimi tulifanya tulichotakiwa kufanya, upande wetu tumetimiza kwa asilimia 200 Dunia imeona, sijui kama na wewe umetiza yako’ – Vunja Bei.

Frank & I did what we did, upande wetu tumetimiza kwa 200% dunia imeona, sijui kama na wewe umetimiza yako kama ilivyo sasa umekua mkubwa hatujawahi kula hata senti ya kazi yako ili ujijenge zaidi’ – Fred Vunja Bei.

‘Viongozi hula mwisho, tumekubali uwe huru ilimradi tumekupa msingi huwezi kulala njaa au kulala nje na hautalipa chochote sababu tunakuthamini na wewe unatuthamini inatosha, hutokosa madini yoyote kutoka kwetu, Unaweza kwenda Kijana One Love’ – Vunja Bei.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *