Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amiri Mkalipa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amewatoa hofu wafanyabiashara pamoja na wachimbaji wa madini jijini Mwanza kuhusu usalama wa uwekezaji wao wanapoamua kuwekeza katika soko la hati fungani kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini na biashara, Mkalipa alisisitiza kuwa Serikali imeweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha uwekezaji wote unakuwa salama na wenye tija kwa wananchi.

Alieleza kuwa Mkoa wa Mwanza umeendelea kuwa kinara katika ununuzi wa madini nchini, sambamba na juhudi kubwa zinazofanyika kudhibiti utoroshaji wa madini, jambo ambalo limeongeza mapato ya Serikali na kuimarisha uchumi wa mkoa huo.
Kwa upande wao, waratibu wa kikao kazi hicho kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), akiwemo Fideus Mkate, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha, pamoja na Kennedy Mwasanga, Mchambuzi wa Masuala ya Fedha, walisema lengo la kuwafikia wadau hao ni …


