Kuwa na mwili mkubwa au kibonge, sio sababu ya kushindwa kupendeza hasa wewe dada!! Dhana hiyo nakuambia ondoa kuanzia leo hii kwa kuwa nitakupa sababu za kwanini upendeze.

Miongoni mwa sababu za wewe dada mwenye mwili mkubwa/pulse size unatakiwa kuzijua ili upendeze basi ni kujua aina ya mwili wako yani umbo lako na madhaifu yake. Mfano unajua umejaaliwa tumbo basi hakikisha nguo zako hazibani tumbo/kuchora tumbo lango.
Mbili epuka kuvaa nguo zinazoenda na wakati yani sio lazima kila msimu wa nguo Fulani umetoka basi uwe nayo. Kuna zingine zitakataa kulingana na mwili wako hasa hizi crop top na short bike tight/ taiti fupi.
Rangi, hakikisha rangi ambazo zinaweza kuchora mwili wako uzipate kwenye ngu zile kubwa kubwa au tafuta rangi nyeusi.. hii inaficha vyema madhaifu ya mwili kama vile tumbo,nyamaza mgong’o na n.k.
Makoti.. najua kuna makoti ya ofisini na yale ya jeans au laser jacket, hapa unaweza kuwa mchaguzi mzuri sana hasa kwenye haya ya ofisnini, hakikisha unapata ambalo linakuenea yani halibani mikono wala halishindi kufika mbele/kufunga.. Na kwa yale ya jeans/laser basi epuka kuchagua yaliyo namba ndogo kwako na yaliopauka rangi.
