Harmonize atamba kusumbua watu vichwa

Msanii wa muziki Hamonizeameendelea kujigamba kuwa ngoma yake ya ‘Single Again’ bado inafanya vizuri na ipo kwenye orodha ya ngoma 10 zinazofanya vizuri Spotify Afrika, baada ya kusema hayo harmonize ameendelea kusisitiza ujio wa albamu yake mpya na ya nne wakati wowote.

“Sijui mnakulaga nini, ila ngoja niweke sawa mambo na wasambazaji wangu wa kazi, kisha niachia albamu yangu!! Nasemaje labda muende kuisumbua Mahakama ila hukumu iko pale pale,”ameandika msanii huyo Instastory yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *