Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan kutangaza siku tano za Maombolezo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kilichotokea siku ya jana Februari 10, Staa wa muziki Bongo, Harmonize ameweka wazi kuungana na Rais Samia kuomboleza kifo hicho hivyo ametangaza kusitisha kutumbuiza kwenye tamasha ambalo lilipangwa kufanyika leo katika viwanja vya Zakhem Mbagala, Jijini Dar Es Salaam.
Harmonize ametoa taarifa hiyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.