Harmonize apokelewa na mamia ya watanzania

Mwimbaji na Staa wa muziki Bongo, Harmonize   amewasili Nchini Tanzania akitokea Marekani alikoshinda Tuzo tatu za AEAUSA ambazo ni Artist of the year 2023, Best Music Video (single again) na King of The East and Bongo Afro Bongo Flavour.


Mara baada ya kufika katika uwanja wa Kimataifa wa J.K.Nyerere alipokelewa kwa furaha na Katibu Mtendaji BASATA Dkt. Kedmon Mapana Pamoja na viongozi wengine wa BASATA, hata hivyo Waandishi wa habari na Mashabiki wake walikuwa wamejitokeza kwa wingi katika kumpokea Msanii huyo katika Uwanja wa ndege mara tu baada ya kuwasili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *