Staa wa muziki na CEO wa Lebo ya Konde Gang, Harmonize_tz ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kufanya kazi na Hanstone ambaye awali alikuwa akitarajiwa kujiunga na lebo ya WCB.
Katika post yake aliyoweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, leo Fwebruari 28,2024 Harmonize amesema anaumia kuona kipaji kama Hanstone kikipotea hivyo anawaza afike Chama la Konde Gang.
“Can we let really talent die Au tumuunganishe Na Chama Linalo Mtegemea MUNGU ❤️🙏 @kondegang CALL ME ⭐️ @thehanstone🙏🏽,” ameandika Hanstone.