Wikiendi iliyopita mtu mzima Diamond Platnumz aliweka wazi kujivunia kumtoa kimuziki Harmonize kama ambavyo wengi tunaweza kuwa tunakumbuka Diamond alivyomtambulisha msanii huyo 2015 kupitia ngoma ya Aiyola.

Lakini Kauli ya Dimond imeonekana kumkera sana Harmonize ambaye ameipeleka kauli hiyo kwa msanii wake wa Konde Music Worldwide Ibraah kwa kumwambia pia “Nimekutoa”.
Ibrah alikuwa msanii wa kwanza kutambulishwa na lebo ya Konde Gang mwaka 2020 na akiwa chini ya Lebo hiyo aliachia EP yake ya kwanza iitwayo STEPS.
Baada ya hapo wakafuata wasanii Country Boy, Kill na Chid pamoja na Anjela, ila kwa sasa hawa wote ho hawapo amebaki Msanii Ibraah pekee.