Mrembo kutoka Uganda -Rwanda, ambaye anafanya muziki Laika Umuhoza maarufu kama Laika Muisc amefunguka kuwa staa wa muziki Harmonize alim-DM Instagram 2020 na wakabadilishana namba ila walikuja kukutana 2023 na akampeleka Zanzibar.
Akifanya mahojiano na Galaxy TV, Laika anabainisha kuwa staa huyo wa Tanzania alilipia kila kitu mpaka yeye kufikaTanzania na wakawa wote kisiwani Zanzibar na jijini Dar Es Salaam.
Laika pia anafafanua kuwa safari yao haikuwa ya kimapenzi bali ilikuwa ni ya kikazi zaidi kwani aliondoka Bongo akiwa na mtayarishaji wa muziki B-Boy kwa ajili ya kurekodi kazi zake.