Staa wa muziki nchini Harmonize ameweka wazi kuwa hii ni mara yake ya kwanza kwenda kanisani, na anafanya hivi kwaajili ya mpenzi wake mpya ambaye ni Poshy.

Harmonize amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia ameshre video akiwa kanisani.
Pia Harmonize ameonyeshwa kushangazwa na namna watu mbalimbali wanaomshangaa yeye kuingia kanisani leo.
Kwenye insta stories Harmonize amesema ‘inachekesha kuona watu wanasema nimekosea kupelekwa Kanisani na mpenzi wangu, Lakini wewe Mpenzi wako anakuchukua anakupekeleka kwenye sehemu za sherehe kila siku ambako hakuna Mungu eneo hilo. Kizazi kinasikitisha sana hiki, Naamini Kwenye Mungu mmoja’ – Harmonize

Ikumbukwe staa huyo wa ‘Single Again’ amewahi kuwa na mahisiano na Kajala, amabye pia alikuwa muumini mzuri wa kwenda kanisani na wakati mwingine walikuwa wakipigia picha kabla ya kwenda kanisani.