Visiwa vya Cape Verde, ndipo panatajwa alipo rapa Diddy ambaye anatajwa kukimbia nyumba zake kufuatia maofisa usalama kuvamia nyumba zake za Los Angeles na Miami usiku wa kuamkia leo.
Diddy ametajwa kutumia ndege yake binafsi aina ya Gulfstream 5, kwenda kwenye visiwa hivyo. Ila mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi kuwa rapa huyu yupo humo licha ya kuonekana uwanja wa ndege wa Miami saa kadhaa baada ya maafisa kuvamia kwake.