Na Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.
Serikali Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, imesema kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29 mwaka huu imejipanga kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao, na kuwataka wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura kwa uhuru na amani
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Halmish Azal na kuongeza kuwa wataimarisha ulinzi na usalama katika uchaguzi mkuu hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kuchagua viongozi watakao ongoza kwa miaka mitano ijayo.

Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema wamejipanga kupiga kura kwa amani na utulivu ili kupata viongozi watakao waletea maendeleo.
Kwa upande wao viongozi wa dini wilayani humo wametoa wito kwa wananchi kujitokeza siku hiyo ya tarehe 29 Oktoba kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi na kuendelea kuitinza amani ya nchi.


