Hamad Hamis Kocha Mkuu Tz Prison

Tanzania Prisons imetangaza kumteua Hamad Hamisi Ally kuwa kocha mkuu klabuni hapo kwa mkataba wa miaka 2 akichukuwa mikoba ya Fredy Felix Minziro aliyeoneshwa mlango wa kutokea.

Hamad amewahi kuwa kocha msaidizi chini ya kocha Mkuu Etienne Ndayiragije tangu wakiwa Mbao fc ya Mwanza na baadae KMC FC akasalia kuwa Kocha Mkuu wa muda KMC baada ya Ndayiragije kwenda Azam FC.

Baada ya KMC kumteua Hitimana kuwa mkuu, Hamadi Hamisi Ally aliendelea kuwa kocha msaidizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *