Halmashauri wilaya ya Kishapu kuupokea Mwenge wa Uhuru

Jumla Ya Miradi Ya Maendeleo 41 Inarajiwa Kuzinduliwa Na Mingine Kuwekewa Mawe Ya Msingi Katika Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Zinazotarajiwa Kuanza Kesho Katika Mkoa Wa Shinyanga.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ofisini Kwake Leo Julai 26 2023 Kuhusiana Na Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga Christine Mndeme Amewataka Wakazi Wa Mkoa Wa Shinyanga Kujitokeza Kwa Wingi Katika Mapokezi Ya Mwenge Huo Hapo Kesho Ambapo Utapokelewa Katika Shule Ya Msingi Buganika Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Kishapu.

Mwenge Wa Uhuru Ni Moja Kati Ya Alama Za Uhuru Wa Taifa La Tanzania Na Hukimbizwa Kila Mwaka Hapa Nchini Kwa Lengo La Kuwaunganisha Watanzania Sambamba Na Kuzindua Miradi Mbalimbali Ya Maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *