Baraza la Madiwani, watumishi wa Umma na viongozi wakuu wa Halmashauri za Momba kutoka mkoani Songwe na Makete kutoka mkoa wa Iringa wametembelea katika halmashauri ya Manispaa ya Tanganyika mkoani Katavi Kwa Lengo la kujifunza biashara ya Kaboni.
Mateo Emanuel Chikoti, Mwenyekiti wa Wilaya ya Momba ameeleza kuwa dhumuni kubwa ni kuja kujifunza njia Bora za uhifadhi misitu na biashara hiyo ya Kaboni ili na wao wakaitoe elimu hiyo Kwa wananchi hasa katika vijiji vilivyozungukwa na misitu wilayani Momba.

“Awali ya yote tumekuja kujifunza, wezetu ninyi najaribu kuvuta hisia na ninakutana na mandhari ya Kilimanjaro wakati nipokwenda kutembelea na kujifunza mradi wa umwagiliaji kwamba Kila ukipita unakutana na kijini, kijani kijana Sasa mazingira haya yanatuvutia kweli kweli na ndio maana watu wengi wanakuna sana huku, hongereni sana” amesema Bwana Mateo Emanuel.
Aidha Hamadi Mapengo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesisitiza kuwa biashara hiyo inahitaji kujituma kwa umoja kwani ni biashara yenye changamoto sana hususani katika utekelezaji wake unahusisha sehemu ya misitu ambayo inajitosheleza, hivyo basi mnaweza kutofautiana na wananchi wanao vamia misitu ambao pia ndio wapiga kura.

Sambamba na hayo bwana Shabani Juma Juma Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika ameelezea hatua na mbinu walizotumia kufanikisha biashara hiyo huku akisema” baada ya biashara hii yakaboni tilipima ardhi na kutenga kiasi cha hekari elfu arobaini na saba (47000) kwaajili ya kilimo na Kuna mashamba tumeyauza Kwa hiyo karibuni sana kuwekeza mkoani hapa,” amesema Shabani.
Akiendelea kubainisha Mkurugenzi Mtendaji wa Tanganyika pia ameongeza kuwa wameshapata wawekezaji wakubwa licha ya uwepo wa changamoto ndogo ndogo ambazo ziko njiani kutatuliwa na shirika la Serikali la (ASSA) huku akiongeza kuwa Kuna maeneo Kwa ajili ya wawekezaji wa kati, maeneo kwaajili ya viwanda yote yametokana na mafanikio ya biashara ya Kaboni.

Akihitimisha mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amesema kuwa kwanafasi hii mliyoipata ya kuja kujifunza wanao mchango mkubwa wa kuufanya Kwa jamii.
“Maafisa mipango, wenyeviti na wakurugenzi ili biashara hii ifanikiwe inahitaji kujikana nafsi, kwani Kuna baadhi yenu hutumia pesa za miradi kujinufaisha wao wenyewe, rushwa lazima muiogope, mkiwa na eneo kwaajili ya biashara ya Kaboni halafu mmoja wenu ambae pia yupo humu kaja kujifunza akiwa sio mwaminifu hamtafanikiwa” amesema Buswelu


