Mshiriki wa shindano la Miss World kutoka hapa Nyumbami Tanzania, Halima Kopwe anaongoza kwenye zoezi la kura kupitia website ya Miss World.
“Hadi sasa, tumeweza kushikilia namba moja kwa kura kwenye upande wa website visits. Ili kuniwezesha kubaki kileleni, tembelea website ya miss world iliopo kwenye bio yangu na kufuatilia matukio yangu mara kwa mara,”ameandika mrembo huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kwa sasa mrembo huyo yupo nchini India ambapo shindano la ulimbwende la dunia (Miss World),linatarajiwa kufanyika ifikapo Machi 09,2024.