HALI YA USALAMA UTENDE NI SHWARI, SUNGUSUNGU WAPEWA TANO 

Daniel Gahu, Itende – Katavi.

Wananchi katika Kijiji cha Utende Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamesema uwepo wa jeshi la jadi maarufu kama sungu sungu kijijini hapo umesaidia kuimarika Kwa usalama kijijini hapo.

Hayo yamesemwa wakati wa maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa jeshi hilo yaliyofanyika katika Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. 

Salala Chagu, mkazi wa Kijiji cha Utende amesema uwepo wa Jeshi la Sungusungu limeimarisha ulinzi maradufu kwa wananchi. 

”tunashukuru sana jeshi la Sungusungu majambazi yamepungua wezi wamepungua tunashukuru sana sungusungu yetu na serikali yetu’,” ameeleza Salala.

Katika hatua nyingine amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano ulipo baina ya Jeshi la Polisi na Mkuu wa Wilaya ya Mlele. 

Rafaeli Opita, Mtendaji wa Kijiji cha Utende akisoma taarifa ya utendaji kazi ya jeshi la sungusungu amesema jeshi hilo limejipanga kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwaajili ya kuanzisha ujenzi wa zahanati kwenye kijiji hicho ili kuepusha wananchi kufuata huduma za matibabu katika kijiji mama cha Utende.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga amelipongeza jeshi hilo kwa kuendelea kuimarisha ulinzi kwa wananchi huku akiliomba jeshi hilo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama pia kuendelea kuimarisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *