Taarifa mbalimbali za Vyombo vya Habari, bado zinaeleza kuwa hali ya Papa Francis (88), ni mahututi na vipimo vya damu vilionesha figo zake zimeshindwa kufanya kazi huku Daktari wake akisema anasumbuliwa na maradhi ya nimonia na maambukizi ya mapafu.
Katika sasisho la hivi karibuni, Vatican ilisema Papa Francis hakuwa na shida yoyote ya kupumua tangu alipozidiwa majira ya usiku wa Jumamosi ya Februari 22, 2025 lakini bado alikuwa akitumia oksijeni ya ziada, ili kupumua.

Madaktari wake walisema, “kuna utata wa picha ya kimatibabu, lakini tunaendelea kuhakikisha hali yake inakuwa sawa kwa kumpatia matibabu stahiki kulingana na aina ya matokeo kadri tunavyoendelea kuchukua vipimo.”
Nchini Marekani, Kadinali Timothy Dolan alikiri kile ambacho viongozi wa kanisa huko Roma hawakuwa wakisema hadharani kwamba waaminifu Wakatoliki walikuwa wameunganishwa kando ya kitanda cha Papa wakimuombea apate uponyaji.

“Na hii inatokana na ukweli kwamba Baba yetu Mtakatifu Papa Francis yuko katika hali dhaifu sana ya afya na pengine karibu kufa,” alisema Dolan katika mahubiri yake kutoka kwenye mimbari ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick, ingawa baadaye aliwaambia Waandishi wa Habari kwamba anatumai na anasali ili Papa arudi salama.
Hata hivyo, Madaktari wamesema hali ya Francis ni ya kumuombea kutokana na umri wake, udhaifu na ugonjwa wa mapafu uliokuwepo hapo awali, jambo ambalo limeleta uvumi kuhusu nini kinaweza kutokea ikiwa atakuwa amepoteza fahamu au vinginevyo na hata wengine wakisema ni vyema akajiuzulu.

Aidha, Madaktari hao wameonya kuwa tishio kuu linalomkabili Francis ni maambukizi makubwa ya damu ambayo yanaweza kutokea kama matatizo ya nimonia na hadi leo hakuna marejeleo ya mwanzo katika sasisho za matibabu zilizotolewa na Vatikani.
Inaarifiwa kuwa mwishoni mwa wiki alikutwa na vipande vinavyofanana na seli ambavyo huzunguka kwenye damu vinavyosaidia kutengeneza damu kuganda, ili kuacha kutokwa na damu au kusaidia majeraha kupona.

Papa Francis pia alipata upungufu wa damu na wakati wa kuongezewa damu alipewa matibabu ili kuongeza kiwango cha hemoglobin katika damu yake, ambayo husaidia damu kubeba oksijeni zaidi utaratibu ambao unadaiwa ulikuwa na manufaa.
Itakumbukwa kuwa Desemba 2024, Papa Francis aliteuwa Makadinali wapya 21 na mmoja wao alikuwa chini ya umri wa miaka 80 wote wakistahili kupiga kura katika mkutano wa kumchagua mrithi wake.

Ongezeko lao lilileta jumla ya idadi ya makadinali wenye umri wa kupiga kura kufikia 140, zaidi ya kikomo cha wapatao 120 kilichowekwa na St. John Paul II, lakini wapiga kura kadhaa wa sasa wanatimiza miaka 80 mwaka huu (2025), na hivyo kupunguza idadi hiyo.
Maara tu alipokuwa mgonjwa hivi karibuni, Papa Francis aliamua kuongeza muda wa miaka mitano wa Mkuu wa sasa wa Chuo cha Makardinali, Kadinali Giovanni Battista Re (91), akiwa na jukumu muhimu katika maisha ya uongozi wa Kikatoliki, na ni mtu muhimu wakati wa mpito kati ya upapa mmoja na ujao.
