Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Hakuna Tsunami wala utabiri wa kutokea

Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama imekanusha taarifa ya uwepo wa tishio la Tsunami nchini.

Taarifa za uwepo wa Tsunami zilizagaa kwa wingi jana na kuleta taharuki kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

“Hakuna Tsunami na hakuna utabiri wowote wa Tsunami,” ameeleza Mhagama wakati akizungumza na Moja ya chombo cha habari Tanzania.

Taarifa hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii pamoja na video yake, inaendana na taarifa rasmi ya mazoezi ya utayari wa Tsunami yanayoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO yakienda kwa jina IOWAVE23, jina ambalo pia lilionekana katika taarifa hiyo.

Mazoezi hayo yalipangwa kufanyika Oktoba 4, Oktoba 11,na Oktoba 18 na Oktoba 25, katika nchi mbalimbali. Zoezi hili linahusisha nchi zilizopo katika mwambao wa Bahari ya Hindi, kwa mwaka huu likitajwa kuhusisha nchi 25 ikiwemo Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *