Serikali Nchini kupitia Wizara ya Afya, imetangaza kuwa kwasasa hakuna ugonjwa wa Marburg na kuwataka Wananchi kuendelea kuwa huru katika uzalishaji wa uchumi na Maendeleo.
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ametoa kauli hiyo leo Machi 13, 2025 wakati akihitimisha shughuli zote zilizohusu mlipuko wa ugonjwa huo ulioikumba Kata ya Ruziba, Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera Januari 16 mwaka mwaka 2025 na kusababisha idadi ya vifo vya watu wawili.






