Serikali imeweka miongozo ya kusajili laini za Simu kupitia Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, huku ikilendelea kuchukua hatua kwa Matapeli wa Mtandaoni wanaotumia simu kujipatia fedha isivyo halali, kwani hakuna laini za simu zinazosajiliwa kiholela.
Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maryprisca Mahundi ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga ambapo ameuliza Je, Serikali haioni haja ya kuzuia usajili holela wa laini za simu mitaani kutokana na utapeli unaoendelea mitandaoni.
“Miongozo hii inahakikisha kuwa laini zote zinasajiliwa kwa alama za vidole, hivyo kutokuwepo kwa mianya ya kusajili laini kiholela. Hata hivyo, wahalifu wa mtandaoni hutumia mbinu kwa kuwalaghai mawakala na watumiaji ili laini zilizokwishasajiliwa zitumike kwenye uhalifu,” amesema.
“Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TCRA na watoa hudumaza mawasiliano inaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu kupitia njia ya kutoa elimu kwa umma juu ya uhalifu mtandaoni na njia zakujilinda, kuhakiki taarifa za usajili kupitia namba *106#Kutoa taarifa za uhalifu kupitia namba 15040, ilikuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vya udanganyifu.”
Akijibu Swali la Mbunge Sanga ambaye amesema bado vitendo vya utapeli kwa njia ya simu vinaendelea kwa kasi sana ikiwa ni miaka kumi jambo hilo likiongelewa.
“Sisi Kama Serikali hatua kali sana tumeshachukua kupitia TCRA na na utakuwa shahidi pia, wimbi hili limepungua kwa kiasi fulani, maana ilikuwa balaa zaidi ya ambavyo ipo sasahivi,”
“TCRA wanaendelea na namna mbalimbali za kuona kwamba zinadhibiti line ambazo zinapatikana kwa njia ambazo sio sahihi, Kwaio Kama serikali tumeshachukua hatua na kazi Unaendelea,” amesema Mahundi.