Jeshi la Polisi mkoani Arusha, linamshikilia hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo mkoani humo kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mwendesha bodaboda baada ya kumlewesha pombe.
Pamoja na hakimu huyo kushikiliwa, Jeshi hilo pia linamshikilia mwathirika wa tukio hilo kutokana na sheria inayosema kuwa mwanaume anayeruhusu kuingiliwa na mwanaume mwenzake naye atakuwa ametenda kosa.