Polisi Mkoa wa Arusha inaendelea na uchunguzi wa tukio la Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo wilayani Ngorongoro, anayedaiwa kumlawiti kijana baada ya kumlewesha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema Kwa sasa kinachoendelea ni uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa ndiye anaendelea kushikiliwa hadi sasa.
Hadi Februari 3,2024 mbali na hakimu huyo, polisi pia ilikuwa inamshikilia mwathirika wa tukio hilo kutokana na msimamo wa sheria unaotaka mwanamume anayemruhusu mwanamume mwenzake kumwingilia (unnatural), ametenda kosa la jinai.