Baada ya kuwepo kwa uvumi juu ya Mdau wa michezo Tanzania na aliyekua msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara kusemekena anataka kugombea Ubunge Jimbo la Ilala, leo Manara amerudi kwa mara nyingine kulitolea ufafanuzi jambo hilo.
Manara kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ‘Nirudie mara ngapi kusema siwezi kugombea na Mh. @zungumussa nafasi ya Ubunge wa lala?Niseme kwa lugha gani mnielewe?’ – Manara.
Manara ameendelea kwa kusema ‘Heshma yangu kwake ni kubwa mno kuliko hivi vyeo vya kupita. Tumejenga mahusiano makubwa ya kidugu na ya muda mrefu, nitakuwa Mtu wa hovyo mno kushindana nae !!’ – Manara.
‘Najua llala ni kwetu na nna Nasabu kubwa pale, lakini akigombea sithubutu kushindana nae,ni utovu mkubwa wa adabu na kwetu hatujalelewa hivyo !! Hope huu mjadala nimeufunga na ikiandikwa mbele ya safari nitawatumikia Wana Ilala na Kariakoo yake Insha’Allah ..’ – Manara.