HAIDAR ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE SINGIDA MJINI

Na Saulo Stephen – Singida.

Muwekezaji na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kusindika Pamba BIOSUSTAIN Tanzania Limited kilichopo Mkoani Singida, Sajad Haidar Leo Juni 29 ,2025 amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa jimbo la Singida mjini kwa tikeki ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Sajad ambae ni kada wa chama cha Mapinduzi, CCM amechukua Fomu hiyo mbele ya katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Neema Luga katika ofisi za chama hicho wilaya zilizopo soko la msufini Mjini Singida.

Hii ni mara ya kwanza Kwa Sajad kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya Ubunge katika jimbo la Singida Mjini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *