Gutteres Ataka Wafanyakazi 17 wa UN Kuachiliwa Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa wafanyakazi wote wanaoshikiliwa Yemen na maafisa wa serikali ya Kihouthi.

Waasi wanaoungwa mkono na Iran, Jumatatu ya Juni 10,2024 walitangaza kuwakamata wafanyakazi 13 wa Umoja wa Mataifa wakidai kuwa mwajiri wao anahusishwa na idara ya ujajusi ya Marekani, CIA na kwamba wamekuwa wakiendesha operesheni za kijasusi nchini humo kwa miaka mingi.

Wafanyakazi wengine wanne wa Umoja wa Mataifa wamezuiliwa nchini humo tangu walipokamatwa mwaka 2021 na 2023.

Hawajawa na mawasiliano na mwajiri wala familia zao na akizungumza baada ya kukutana na mjumbe maalumu kwa Yemen, Hans Grundberg,Katibu Mkuu Guterres, amesema anapinga madai ya Wahodhi, huku akiwa na wasiwasi mkubwa wa hali za wafanyakazi wanaoshikiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *