Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Geita (GEUWASA), imevunja mkataba na mkandarasi aliyekuwa na zabuni ya kujenga mradi wa maji katika Kata ya Bung’wangoko wilayani Geita mkoani hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Geuwasa, Mhandisi Frank Changawa amethibitisha taarifa hiyo na kudai hatua hiyo inatokana na utendaji usioridhisha wa mkandarasi.
Amemtaja mkandarasi aliyekuwa na zabuni ya mradi huo ni Kampuni ya KELLOGG Construction Limited, ambaye inadaiwa ameshindwa kutekeleza mradi kwa ufanisi na kwa muda uliopo kwenye mkataba.
Amebainisha mradi wa maji Bung’wangoko unatekelezwa kwa gharama ya Sh milioni 569 na utekelezaji ulianza Machi 27, 2023 na ulitarajiwa kukamilika Agosti 30, 2023 lakini mkandarasi huyo ameshindwa.