George Weah akosa Urais wa Liberia

George Weah (57), amepoteza nafasi ya kuongoza ungwe ya pili ya Taifa la Liberia kwa tofauti ya kura 28,000 dhidi ya Joseph Boakai (78) kupitia matokeo yaliyotangazwa jana.
Katika matokeo yaliyotangazwa juzi Novemba 16, 2023 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Boakai alishinda kwa asilimia 50.58 dhidi ya asilimia 49.42 za Weah kupitia wapiga kura 1,431, 388 waliojitokeza katika vituo 4,295 vya kupigia kura.

Baada ya matokeo hayo, Weah kupitia hotuba yake amesema amempigia mshindani wake Boakai na kumpongeza kwa ushindi huo ulioweka historia ya kuendeleza ukuaji wa Demokrasia nchini humo.

Weah amesema ataachia nafasi hiyo kwa amani huku akiwataka wafuasi wake wakubaliane na matokeo ya ushindi wa Boakai aliyemshinda uchaguzi wa mwaka 2017 kwa asilimia 62 ya kura zote. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *