Mahakama ya Wilaya ya Babati, imemwandika wito aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul kufika Mahakamani hapo siku ya tarehe 27 Desemba 2023 Kujibu mashika ya Jinai dhidi yake.
Kesi hii ambayo itakuwa ni ya kwanza kuwa kesi ya Jinai Kuendeshwa na mawakili binafsi badala ya serikali kama tulivyozoea itafungua milango mingine kwa raia kumshitaki mtu yoyote ambaye ametenda Jinai na yupo Serikalini bila kushtakiwa na DPP.
Kulingana na barua ya wito huo iliyogongwa muhuri wa mahakama hiyo, Gekul anapaswa kuripoti mahakamani hapo Desemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ikitajwa