Gekul afutiwa kesi, Wakili akata rufaa kupinga

Desemba 27, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Babati ilipokea taarifa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi ya tuhuma dhidi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Pauline Gekul za kumshambulia na kumdhuru Hashim Ally, Novemba 11, 2023 kinyume na kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.

Baada ya video za Mlalamikaji Hashim Ally, kusambaa mitandaoni akiomba msaada kwa Watetezi wa Haki Za Binadamu ili apate haki yake kwa madai ya kufanyiwa Ukatili na Mbunge huyo wa Babati Mjini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara liliwasilisha jadala la tuhuma za Unyanyasaji katika Ofisi ya DPP kwa hatua zaidi

Aidha, Wakili wa Mlalamikaji katika kesi hii, Peter Madeleka amesema wamekata Rufaa kupinga uamuzi wa DPP kuiondoa kesi hiyo Mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *