Geita yakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu isiyoendana na kasi ya ukuaji wa uchumi

Serikali imesema Mkoa wa Geita bado unakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na ubora wa idadi ya watu husika hali ambayo inapelekea ongezeko la mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya pamoja na elimu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya rais, Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu dunia leo julai 11,2024 yaliyofanyika Mkoani Geita na kuongeza kuwa takwimu ni nyenzo muhimu katika kupanga shughuli za maendeleo ikiwemo sekta ya maji, elimu, afya madini na kilimo ambapo kasi ya ukuaji kwa geita imefikia asilimia 5.4 na uwiano wa umri tegemezi ukiwa asilimia 106.8 huku kitaifa ikiwa ni asilimia 3.2

Aidha Mkurugenzi wa tume ya mipango Anjela Shayo amesema licha ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya watu kwa Mkoa wa Geita hali hiyo imechangia mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kiuchumi huku ikikabiliwa na changamoto ya matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijisia kwa kushika nafasi ya 3 kitaifa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema ongezeko kubwa la watu katika mkoa huo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na serikali kuimarisha zaidi sekta ya afya hali ambayo inapelekea wakina mama wengi kujifungulia katika mazingira mazuri kwani katika kipindi cha awamu ya 6 serikali imekamilisha ujenzi wa hospitali mbili za rufaa katika mkoa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *