GEITA: WACHIMBAJI WADOGO WAJADILI MAENDELEO SEKTA YA MADINI

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameongoza kongamano la Wachimbaji wadogo Nchini lililofanyika kitaifa katika Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro iliyoko Manispaa ya Geita.

Akizungumza katika Mkutano huo wa hadhara, Waziri Mavunde amesema kongamano hilo limekutanisha wachimbaji wadogo kutoka ndani na nje ya mikoa ya kanda ya ziwa huku ajenda kuu ikiwa ni kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.

Amesema kongamano linalenga kujadili, kutangaza na kusherehekea maendeleo ya Sekta ya Madini kwa Wachimbaji wadogo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imeweka sera rafiki kwa wachimbaji.

Kongamano hilo liliandaliwa na Shirikisho la Wachimbaji Wadogo mkoa wa Geita (GEREMA) chini ya usimamizi wa shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA).

Mwenyekiti wa Gerema, Titus Kabuo amebainisha wakati akizungumzia Wananchi na Wakazi wa Mkoa huo na Wageni waliotoka maeneo mbali mbali Kitaifa ambao walihudhuria kongamano hilo.

Kabuo amesema hayo ni matokeo ya juhudi kubwa zilizofanywa na serikali kuboresha mnyororo wa thamani ya kwa wachimbaji wadogo kuanzia mchakato wa uchimbaji, uchakataji na usafishaji wa madini.

“Haya ni mapinduzi makubwa, haya yote yanasababishwa na utulivu uliopo nchini, amani tuliyonayo lakini pia na sera rafiki zinazotujali sisi wachimbaji”, amesema Kabuo.

Katibu wa Wachimbaji Wadogo Wilaya ya Geita, Agnes Kihamba amesema kongamano hilo litajumuisha pia wachimbaji wadogo wanawake ambao wamepata fursa kubwa chini ya serikali ya awamu ya sita.

Amesema hapo awali haikuwa rahisi kwa wanawake kumiliki leseni kutokana na mfumo dume kwenye sekta ya madini lakini kwa sasa mabadiliko yamefanyika na kufungua milango kwa wanawake.

“Leseni zilivyotoka kwa uwingi, imefanya wachimbaji wadogo kuonekana tuna nguvu zaidi kuliko hapo mwanzo, hapo mwanzo tulikuwa hatuna nguvu kwa sababu tulikuwa tunaishi kwa kuvamia maeneo” amesema Kihamba.

Meneja wa Mgodi wa Msasa wilayani Geita, James Matimba amesema kwa sasa wachimbaji wadogo wananufaika moja kwa moja kwa moja na biashara ya madini tofauti na hapo awali walitegemea madalali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *