GEITA: KIBOKO ALIYEJERUHI, KUUWA NG’OMBE AUAWA

Askari wa Wanyamapori, wamefanikiwa kumuuwa Kiboko ambaye amekuwa akileta taharuki, kusababisha majeruhi, kuharibu mazao na kuuwa Ng’ombe watatu katika Kijiji cha Itale kilichopo kata ya Katoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya Wananchi wamesema Mnyama huyo amekuwa akiwasumbua na kuwapa hofu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kujitafutia kipato na hivyo kuathiri shughuli zao za kiutendaji.

“Changamoto kubwa hapa ni hawa wanyama tunaangaika kwa takribani miaka mitano wametuharibia mazao wametuharibia watoto wetu pia hatuchoti maji kwa uhalisia tunahangaika sana inapofika mida ya jioni kwenda kuchota maji,” alisema Mwananchi mmoja Avelina Hoja.

Afisa Wanyamapori msaidizi Daraja la pili kutoka kutoka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Seif Marambo amethibitisha kuuwawa kwa mnyama huyo huku akiwataka wananchi kutopanda mazao yanayoendanda na mnyama huyo kama chakula chake pamoja na kuweka tahadhari wanapokuwa wanaenda kuoga ziwani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Itale, Michael Kongoro amekiri wananchi wako kusumbuliwa na mnyama huyo kwa kipindi cha miaka 5, huku akiwashukuru TAWA kwa kutoa usaidizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *