Gari la abiria lenye namba za usajili T 608 DMP mali ya kampuni ya Batco lililokua likisafiri kutoka eneo la Mwasubuya Wilaya ya Bariadi kwenda Mkoani Mwanza limepata ajali na kutumbukia mtoni katika daraja la Simiyu lililopo katika eneo la Busalanga wilaya ya Magu na kusababisha kifo cha mtu huku watu wengine 24 wakiokolewa.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Wilaya ya Magu Gaston Tibulebwa amesema mpaka sasa ajali hiyo imesababisha kifo cha mwanaume mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika huku wakiendelea kufanya jitihada za kulitoa gari hilo kwani mpaka sasa bado kuna mwili wa mtoto mdogo haijafahamika ulipo.