Fursa za Kiuchumi Uwanja wa Ndege Shinyanga Zaanikwa

Kukamilika kwa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shinyanga unaoendelea katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga kunatarajiwa kutoa fursa mbalimbali za uwekezaji kwa wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa hatua itakayoongeza chachu ya ukuaji wa uchumi wa mkoa.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS)Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu amebainisha hayo kupitia Kikao cha wadau wa Maendeleo Mkoani Shinyanga Kilichoketi katika eneo la Ujenzi wa Uwanja huo kwa Lengo la kuchakata fursa za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa Mradi huo.

 Meneja Mradi kutoka kampuni ya China Hennan International Corperation Group inayotekeleza Mradi huo Bw. Shi Yinlei ameeleza kuwa wanatarajia kukabidhi kwa serikali eneo la kurukia ndege kabla ya mwezi Agosti Mwaka huu na jingo la kusubiria abiria likitarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu na kuelezea changamoto ya mvua kuchelewesha kasi ya Ujenzi huo.

 Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho wameipongeza Serikali kwa Utekelezaji wa Mradi huo wa Kimkakati ambao wameuelezea kwamba utakuwa chachu ya Maendeleo katika kuinua Uchumi wa Mkoa wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa Kwa Ujumla.

Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga unaojengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) na unaosimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia umeanza Aprili 4,2023 na unatarajia kukamilika ifikapo Oktoba 3,2024 (ndani miezi 18) ukijengwa kwa fedha za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) ukiwa umetoa jumla ya ajira 112 ambapo ajira 96 sawa na asilimia 86 zimetolewa kwa Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *